change the language of a blog

CHUYAM CHUYAE: MTOTO WA AISHWARYA RAI AWA MAARUFU KULIKO WAZAZI W...

CHUYAM CHUYAE: MTOTO WA AISHWARYA RAI AWA MAARUFU KULIKO WAZAZI W...:   Aaradhya Bachchan mtoto wa masupa staa wa bollywood aishwarya rai na abshek hawa gumzo sana katika vyombo vingi vya habari huku kila ha...

HUYU NDIYE MUSTAPHA J KIROBOTO, MWANDISHI WA SCRIPT.........KAMA HAUMJUI JARIBU KUMSOMA.


















Wito wa pili ulipenya masikioni kwangu taratibu nakunifanya nifungue macho yangu, sikutambua kwanini nililala, nika kutana na sura ya Anita, binti mrembo sana aliewahi kuwa mpenzi wangu moyo ulini ripuka sana na kuhisi ganzi ikiniandama mwili mzima, Anita alitabasam huku akiwa ameniinamia, kana kwamba alikuwa akisubiri kuongea nami, nilitaka kuamka nikagundua kuwa sikua na uwezo wa kufanya hivyo, kwani nilijihisi kama mtu nisie na mwili, kwa haraka nikajua mwili wangu umekufa ganzi ndio maana siusikii kuni sapot kwa ninacjokitaka, kitu cha ajabu eneo lile lilikuwa limetawaliwa na giza lenye kuzuia nuru ya macho, kuangaza upande wa kulia kwangu nikamuona mzee manata, (Babu yangu mzaa mama,, tuliemzika miaka sita iliyopita) hofu ikanizidi nikaanza kuhisi baridi kali sana maeneo ya kifua, nilipotaka kunyanyua mkono wangu ili nikiguse kifua changu nikajihisi kama sina mikono, Anita alisikitika kisha akaniambia "subiri Amon bado hawaja kuzika" kauli ya Anita ilinifanya nijihisi hali ambayo sikuwahi kuihisi tangu kuumbwa kwangu, Kusema ukweli niliamini kuwa nipo ndotoni, na yale mazingira ya eneo lile nikahisi kuwa ile ni ndoto tena ya kutisha, "Anita" nilimuita kwa sauti ambayo sikuwahi kuiongea, siluelewa ni kwanini kinywa changu kimetoa sauti ile, Anita akanituliza kisha akaniambia kuwa "bado ndugu zako hawajakuzika, hebu tulia ili mwili wako ukufikie ukiwa kamili kwani maisha ya huku ukiwa na upungufu wa kiungo chochote ni tabu sana ndio maana mungu anawarudishia viungo hata walemavu wa duniani pindi wanapifika sehemu hii" sikumuelewa kabisaa, kwani nipo wapi? Nilimuuliza anita Anita akamuangali mzee manata kisha mzee manata akavuka upande wa pili na kunisogezea kitu mfano wa shuka jeusi lililojaa vumbi, punde nikaiona hali ya Dunia kwenye ile shuka na wala haikufanana na sinema bali ilikua ni live, nikaonyeshwa nyumbani kwa baba yangu mzazi watu wakiwa wamejaa sana, wengine wanalia, nikaziona gari zangu tatu zimepaki nje mbele ya gari moja ya kubebea abiria wapo madereva wa magari ya kampuni yangu wanachangishana hela wakiwa na huzuni sana mmoja ameshika kitabu, muda mfupi niliziona gari sita zinaingia eneo lile moja ni gari ya kubebea maiti, nilijiuliza nani amefariki nyumbani kwa baba yangu? nikaamini tukio la msiba ndilo lililonifanya nipoteze faham na kufika eneo nililopo, lakini ni wapi nilipo? mbona pako tofauti na maisha ya kawaida? Wakati naendelea kujiuliza nilishangaa kumuona mke wangu kipenzi, mama furaha akitelemka toka garini kinamama majirani wamemshika akiwa hajiwezi, Analia kupitiliza, Dada zangu na mama yangu nao walikuwa hawajiwezi kwa kulia, tena walilia huku wakitaja jina langu eti nimekwenda nimewaacha, nilishikwa na butwaa nikiwa sielewi ninachokiona kinamaanisha nini, mara tena nikamuona Jeremia mdogo wangu anatelemka garini na kukumbatiana na baba yangu mzazi kisha akazunguruka nyuma ya gari akajiinamia na kuanza kulia, vijana akiwepo dany condacta wa moja ya magari ya kampuni yangu wakamzunguruka na kuanza kumfariji eti ajikaze kazi ya mungu haina makosa, nikawaona vijana kadhaa wameongozwa na kaka yangu mkubwa wakaiendea ile gari ya kubebea maiti, kauli moja aliyoiongea kaka ilinishitua eti alisema "Ndugu yangu kupata mafanikio kidogo tu wamemuondoa Duniani" kisha akaanza kulia, sikuwahi kumuona kaka yangu akilia hata siku moja misiba yote iliyopita, huu msiba ni wanani? Nilijiuliza bila wakunijibu, punde kijana mmoja alitelemsha msaraba ulioandikwa Amin Austane themiss, nilishangaa kuona jina langu kwenye ule msaraba, vijana wengine wakisaidiana na kaka yangu wakaanza kuteremsha jeneza,ila cha ajabu walipolinyanyua tu lile jeneza nika hisi kama nimenyanyuliwa mimi nikiwa ndani ya kitu ambacho siwezi kujizuia kinapoinamia upande mmoja, nilimsikia kaka yangu akisema "bebeni vizuri msiinamishe upande mmoja" mara nikajikuta nimekaa sawa ila nikijihisi kubebwa juu juu bado.

MTOTO WA AISHWARYA RAI AWA MAARUFU KULIKO WAZAZI WAKE

Aaradhya Bachchan mtoto wa masupa staa wa bollywood aishwarya rai na abshek hawa gumzo sana katika vyombo vingi vya habari huku kila hatua moja ikiwa inafatiliwa.
Akiwa amevalia pink alionekana ametokelezea sana, baadhi ya vyombo vya haabari vikiripoti mtoto ni noma na nguo zinamkaa sana.

FILAMU ZA KIHINDI: KAMA HUJAIONA ANGALIA SASA.......JOHNDAY

Ni filamu ya kusisimua sana iliyotaarishwa na  Anjum Rizvi, Aatef A Khan and K Asif huku Ahishor Solomon akiwa mwandishi na muongozaji wa filamu hii.
Kwa upamde wa vinara ni mtu mzima  Naseeruddin Shah huku akiwa na Randeep Hooda,Vipin Sharma, Shernaz Patel, Sharat Saxena na Elena Kazan.
si ya kukosa!!!!!