change the language of a blog

UNAKUMBUKA COUPLE HIZI ZILIZOBAMBA KWENYE LUNINGA



1.MZEE SMALL NA BI CHAU






















Muda mrefu sana wapo pamoja kwenye sanaa,mara nyingi ukimwona mmoja basi mwingine yupo pembeni.Hata baadhi ya matangazo ya biashara wamekuwa pamoja


2.RAY NA JOHARI

Kitambo sana tangu Kaole kwenye tamthilia hadi sasa,kwa kweli walikuwa wanabamba sana.

3.NORA NA DR.CHENI
 


Duuuh! kitambo sana enzi za kaole hizo,jamani tumetoka mbali,enzi za TV moja mtaa mzima.

3.BISHANGA NA WARIDI

















4.RICHIE NA AISHA WA MAMBO HAYO















Natamani hawa watu wafanye kazi mapema,mambo haya ni moja ya kikundi cha sanaa kilichokuwa kinabamba sana

MUAROBAINI WA BONGO MOVIES



Tansia ya filamu nchini Tanzania inakabiliwa na changamoto nyingi sana ikiwemo wizi wa kazi za wasanii unaofanywa na watu wachache waopenda kudandia treni kwa mbele.pamoja na hilo lakini suala la wasanii kuuza hati miliki za kazi zao kwa wasambazaji nalo ni tatizo kubwa sana kwani inawanyonya sana wasanii.
Baraza la sanaa Tanzania(BASATA),bodi ya filamu pamoja na mamlaka ya mapato Tanzania(TRA) kwa pamoja wakiwa wanatekeleza azma ya serikali ya kutetea na kuhakikisha haki stahiki za wasanii zinaendena sambamba na kazi nzito wanazozifanya wamesema "MUAROBAINI WA WEZI WA KAZI ZA WASANII TAYARI UMESHAIVA"
Utekelezaji rasmi utaanza januari mosi 2013.
 

KUTOKA BOLLYWOOD:KATRINA KAIF USIKU USIKU KWA RANBIR KAPOOR

RANBIR KAPOOR & KATRINA KAIF




















Hakuna ubishi kwa mastaa hawa wa filamu mpya ya Ek Tha Tiger,Salman Khan na Katrina Kaif hawana tena mahusiano ya kimapenzi,lakini swli lina kuja,Katrina na Ranbir Kapoor je?















Katriina na Ranbir walionekana saa 8 usiku wakiwa pamoja katika makazi ya Ranbir,hali inayolea minong'ono mingi sana kwa mashabiki na wapenzi wao na wengi wao wakitamani wawili hawa kuwa pamoja kwani wanapendezana
.

SAJUKI NA WASTARA "GOLDEN COUPLE" MFANO WA KUIGWA



Nadiliki kuwaiwaita wawili hawa kuwa ni "golden couple" wa miaka 10 na naamini hata wewe unakubaliana na mimi.SAJUKI(Juma kilowoko) na WASTARA ni moja kati ya wanandoa ambao ni mfano wa kuigwa duniani kote.Ndoa kama ndoa pindi wawili wnapoamua kuliendea suala hili huwekeana ahadi nzuri nzuri na naamini hakuna hata ahadi ya kukimbiana pindi mambo yatapoenda mlamba basi tukimbiane,lakini ni wangapi wanaweza kutimiza ahadi za kuishi pamoja kwenye shida na raha?
Mwanzo wa mahusiano ya Sjuki na Wastara yalitokana na mashimo ya maumivu huku kila mmoja akijitahidi kuyafukia,ila tatizo ni kwa namna gani wanaweza kufukia mashimo hayo.Wakati kila mmoja akitafuta naama sahihi ya kufukia mashimo ya maumivu ya mioyo yao yaliyosababishwa na wenzi wao wa zamani,ukaribu ukawasogeza na kijiona wana kila sababu ya kuwa pamoja na kushirikiana kufukia mashimo ya maumivu,basi na mwenyezi mungi ilisha kadilia yake mawili hawa wakawa wapenzi.
Bwana Sajuki akufanya ajizi ailpeleka posa nyumbani kwa Wastara kuhidhinisha uhalali wa kuwa wachumba.
Moja kati ya matukio ambayo kamwe hawawezi kuyasahau ni ajali ya pikipiki,siku chache kabla ya ndoa hali iliyosababisha Bi.Wastara kukatwa mguu,hofu ikiwa imemtanda,"je Sajuki atanioa na hali yangu ikwa kama hivi?"
Mwanaume kamili husisima na msimo sahihi na maamizi sahihi,bila kuyumbishwa Sajuki alisimama na kuhakikisha Wastara ndiye mwanamke wa maisha yake,ndoa ikafungwa

 


.
Maisha yao ya ndoa yalikuwa mazuri sana hali ambayo ilitafsiliwa na nyuso zao zilizo na furaha muda wote.Bibi akiwa producer wa movies.bwana director,kazi mtindo mmoja.
Mwenyezi huwapa mitihani waja wake anaowapenda,Sajuki alipata mtihani wa maradhi yaliyomsumbua sana na kubadilisha kabisa hata muonekano wake.Watanzania wake kwa waume kila mtu katika nafasi yake alimwombea Sajuki kupona na huku wengine wakitoa michango ya hali na mali.Mwanamke imara,mfano wa kuigwa,Bi.Wastara alisimama imara bega kwa bega kuhakikisha kwa hali yeyote na gharama yeyote ile mume wake anapona.Kusema ukweli alionyesha juhudi ya hali ya juu kusimamia afya ya mumewe kipenzi tena huku akiwa ni mjamzito.






















Mwenyezi mungu yu pamoja na wenye kusubiri,Sajuki afya yake ikarejea na sasa yuko fiti kalikiti na sasa wana mtoto.

















Ndugu wasomaji hebu niambieni wawili hawa hawastahiki kuitwa "GOLDEN COUPLE" WA MIAKA 10?
UPENDO na UVUMILIVU ni silaha ya ndoa.
Ndoa nyingi zinavunjika kwa sababu wanandoa wengi wana nunua ndoa,huingia wakiamini magari,nyumba na pesa huweza nunua furaha ya ndoa,kumbe wamesahau mapenzi ya kweli ndiyo msingi wa kila kitu.
Kama mnahitaji ushauri mnaweza waona hawa golden couple.

MAHUSIANO YALIYOZUA GUMZO BOLLYWOOD



aishwarya rai with salman khan Bollywoods most famous break ups!
Salman Khan and Aishwarya Rai:
Walikuwa wapenzi kabla ya ASH kuolewa na Abhishek Bachchan,kuvunjika mahusiano yao kulikuwa ghafla sana na kila mtu hakutalajia kama meli ingeenda mlama.

Ness Wadia Preity Zinta Bollywoods most famous break ups! 
Ness Wadia & Preity Zinta
Mara nyingi walionekana wana furaha sana na wengi wetu tulijua wangefunga ndoa punde si punde lakini mambo yalikuwa kinyume na matarajio ya wengi,mahusiano yalifunjika.


ranbir kapoor deepika padukone Bollywoods most famous break ups! 
Ranbir Kapoor & Deepika Padukone
Mahusiano ya wawili hawa yalitawaliwa na vyombo vya habari,kila hatua yao moja ilikuwa katika luninga na kiukweli walipendezana sana.Lakini mtoto wa mama,RANBIR alitangaza kuachana na mrembo huyu kutoka BOLLYWOOD,Deepika.Katika kipindi cha KOFFEE with KARAN,Deepika alifunguka na kusema Ranbir alikuwa anam-cheat.


karishma kapoor and abhishek bachan Bollywoods most famous break ups!
Karishma Kapoor and Abhishek Bachchan
Inasemekana wazazi wa pande zote walikuwa kikwazo kikubwa cha wawili hawa kuwa mwili mmoja.Jaya Bachchan, mama wa Abhishek na  Babita,mama wa Karishma.

5 BEST BODIES BOLLYWOOD

hrithik 2 Bollywoods top 5 actors with best bodies!
1. Hrithik Roshan
jhon abrahum Bollywoods top 5 actors with best bodies!
2. John Abraham
salman khan 2 Bollywoods top 5 actors with best bodies!
3. Salman Khan
ranveeer singh Bollywoods top 5 actors with best bodies!
5. Ranveer Singh

BONGO MOVIE:MRITH WA KANUMBA HUYU HAPA



































story: SETH BOSCO
starring: ROSE NDAUKA,RAMMY GALIS,SETH BOSCO and ABDALLAH MKUMBILA
produced by: KANUMBA THE GREAT FILM
directed by: ZAKAYO MAGULU
distributors: STEPS ENTRTAIMENT

HOLLYWOOD:MOVIE MPYA SEPT.2012

















starring:
Bruce willis
Joseph Gordon-levitt and
Emily Blunt
 

BOLLYWOOD:MOVIE MPYA SEPTEMBER 2012

Heroine - Hindi Movie
Heroine   Release Date : 21,Sep 2012
About Movie
DirectorMadhur Bhandarkar
ProducerRonnie Screwvala, Madhur Bhandarkar
StarringKareena Kapoor, Arjun Rampal, Arunoday Singh, Shahana Goswami



ATA PATA LAPATA - Hindi Movie
ATA PATA LAPATARelease Date : 21,Sep 2012
About Movie
DirectorRajpal Yadav
ProducerRajpal Yadav
Starring



English Vinglish - Hindi Movie
English VinglishRelease Date : 21,Sep 2012
About Movie
DirectorGauri Shinde
ProducerR. Balki, Rakesh Jhunjhunwala, R.K. Damani
StarringSridevi, Mehdi Nebbou, Priya Anand, Adil Hussain



TRAP - Hindi Movie
TRAPRelease Date : 24,Sep 2012
About Movie
DirectorSafdar Aah
ProducerS B Rana
StarringShahwar Ali, Govind Namdeo



? (A Question Mark) - Hindi Movie
? (A Question Mark)Release Date : 24,Sep 2012
About Movie
DirectorAllyson Patel, Yash Dave
ProducerPercept Picture Company
Starring



Cover Story - Hindi Movie
Cover StoryRelease Date : 26,Sep 2012
About Movie
DirectorLaurence Postma
ProducerSunitha Ram
StarringSunitha Ram, Laurence Postma , Ram Samtani, Pappee Sangtani



Kamal Dhamal Malamaal - Hindi Movie
Kamal Dhamal MalamaalRelease Date : 28,Sep 2012
About Movie
DirectorPriyadarshan
ProducerPercept Picture Company
StarringNana Patekar, Shreyas Talpade, Paresh Rawal, Rajpal Yadav, Om Puri, Asrani, Shakti Kapoor, Anjana Sukhani



Omg oh my god - Hindi Movie
Omg oh my godRelease Date : 28,Sep 2012
About Movie
DirectorUmesh Shukla
ProducerAkshay Kumar, Ashvini Yardi, Paresh Rawal
StarringParesh Rawal, Mithun Chakraborty, Akshay Kumar, Sonakshi Sinha, Prabhu Dheva



Enemy - Hindi Movie
EnemyRelease Year : Sep 2012
About Movie
DirectorAshu Trikha
Producer
StarringSuniel Shetty, Mahaakshay Chakraborty, Mahesh Manjrekar, Mithun Chakraborty, Zakir Hussain, Mumaith Khan, Uvika Chaudhary, Kay Kay Menon, Johnny Lever

KHANS KUCHEZA MOVIE PAMOJA

kutoka kushoto ni salman khan,shahrukh khan,aamir khan na karan johar


















Wapenzi wengi wa filamu Bollywood wanatamani sana KHANS(Shahrukh,Aamir na Salman Khan)kucheza movi pamoja,wakati muandaaji wa movi India Karan Johar alipoulizwa juu ya kuwakutanisha watatu hawa pamoja alisema,"kama nitatengeneza movi ya namna hiyo basi nitaishia hospitali(huku akicheka
).Hakuna stori nyingi za kuwakutanisha ma-super star kama hawa.
Pamoja na maneno haya ya Karan Johar,bado watu wengi wanakiu kubwa na shauku ya kuwaona watatu hawa wanatamba BOLLYWOOD.

TINO AJA NA BONGO MOVIE STAR SEARCH



SUPER STAR wa BONGO MOVIE,Hissan Muya al-maaruf TINO ameamua kuandaa shindano linalokwenda kwa jina la "BONGO MOVIE STAR SEARCH" ili kusaka vipaji vilivyojichimbia Tanzania kote.
Usajili wa kazi yake hii tayari ameshaufanya na sasa full kibali akisubiria kuanza kwa kazi yake hii ambayo ilikuwa IDEA ya pamoja na marehemu KANUMBA.

 Tino ni miongoni mwa wasanii wanatendea haki tanisia hii ya filamu bongo,amekuwa hakifanya vizuri sana katika filamu mbalimbali anazocheza.





SHAHRUKH KHAN NA KATRINA KAIF WALA BATA LONDON


















King of Bollywood,Shahrukh Khan pamoja mrembo anayebamba kwa sasa Bollywood Katrina Kaif wameonekana wakijivinjali jijini London last week,vyombo vingi vya masuala ya movie vimekuwa vikiweka dauti kuhusiana na ukaribu huo ambao siku za karibuni umekuwa ukishamili sana kiasi cha kwamba kutoka holiday London,wawili hao hawakuwa pekee yao hali inayofanya wasiwasi kwa wapenzi wa Bollywood kupungua.Khan alikuwa pamoja na famila yake huku Katrina akiwa karibu na familia hiyo.















Ukaribu wa Khan na Katrina huwenda umesababishwa na Yash Chopra,muandaaji wa filamu mpya ya "JAB TAK HAI JAAAN" iliyowaakutanisha wawili hawa."kikukweli tunaisubilia kwa hamu kubwa sana hii movie"alisema shabiki mmoja wa Khan nchini USA.
Watu wengi hususani wapenzi wa bollywood wamekuwa na shauku kubwa na movie mpya ya KING KHAN na Katrina Kaif ambayo siku chache zijazo itakuwa sokoni.