change the language of a blog

MOOST JAY KUNYANYUA VIPAJI




Moost jay si mwingine ila ni director wa tamthilia ya GREEN MESSAGE inayorushwa na luninga ya TBC1,Moost Jay yupo katika mipango ya kunyanyua vipaji vya waigizaji Muheza-Tanga.Mkurugenz mmiliki wa kampuni ya Moost jay entertainment  Bw. Mustapha j kiroboto (Moost jay)  amejipanga kunyanyua vipaji  vya wasanii wa kuigiza walioko wilayani muheza mkoani Tanga. Akiongea na mtoa habari wake Moost jay amesema kuwa anaamini kuwa mikoa mingi ina vijana wenye uwezo wa vipaji mbalimbali ila tu wadau wengi wa sanaa wameisahau na kujiwekeza Dar peke yake,"awamu yangu ya kwanza nimeanzia muheza lakini pia nitaitazama mikoa mengine kama morogoro, kilimanjaro nk. Licha ya vipaji pia Tanga ina mandhari nzuri kwa kutengeneza michezo yenye muonekano wa kiafrika. Mustapha ana mpango wa kutengeneza Tamthilia kali inayohusu maisha ya watu waishio nje ya miji mikuu, mistuni na kwenye majabari.. Tamthilia hii ina tabiliwa kuja kuchukua nafasi kubwa katika luninga zote Afrika. Jina la Tamthilia hyo litatangazwa muda si  mrefu. Big up moost jay  God bls u. Nae mmoja wa viongozi wa makundi ya sanaa yaliyopo Muheza, Bw.  Wiliam Kiboloma (B4B) amesema kuwa wao wako tayari kushirikiana na kampuni ya Moost jay entertainment katika mpango huo ili kuonyesha wadau kuwa hata mikoani vipaji vipo, B4B amewaomba pia wadhamini wengine kufuata mfano wa  moost jay.