change the language of a blog

CHENNAI EXPRESS YATOA FUNDISHO BONGO MOVIE

Chennai express ni filamu gumzo nchini India kutoka katika kiwanda cha filamu cha wajanja wa town BOLLYWOOD. Filamu hii imeongozwa na muongozaji maarufu wa filamu za mapigano ROHIT SHETTY huku Deepika na Shahrukh Khan wakiifanya filamu hii kuwa kivutio kikubwa mpaka kuvunja record ya mauzo nchini hapo.
Pamoja na hayo yote, wasanii wa BONGO MOVIE  pamoja na wadau tunajifunza nini?.
Muda uliotumika kuitangaza hii filamu si chini ya miezi kumi na ndio sababu ikafanya watu wengi kuisubilia kwa hamu kubwa. Hali ni tofauti kwa hapa bongo, kila mwezi kampuni au msanii anatoa filamu mpya, hamna promo labda posters chache katika vibanda vya vituo vya basi tu. Bado hatupo serious na kazi kiukweli bado sana.
Baada ya chennai express Shahrukh anatoa filamu mpya " happy new year" itakayotoka mwezi wa 10 mwaka 2014