change the language of a blog

HII NDIYO SABABU YA DIAMOND KU-SHINE, WENGI WASEMA NI NJIA ILE ILE YA MAREHEMU KANUMBA

Ni ukweli usiofichika nyota wa bongo flava, kijana Diamond ni msanii aliye na mafanilio sana katika kazi yake hali inayomfanya kuwa gumzo katika vyombo vya habari nchini. Baada ya kuachia video yake mpya iliyofanywa kwa gharama ya  takribani milioni arobaini na tano za kitanzania, mwanamuziki wa muziki wa kizazi kipya Diamond Platnumz amefananishwa na marehemu Steven kanumba kwa jinsi anavyothubutu kufanya mambo makubwa kukuza Sanaa na kipaji chake tofauti na wasanii wengine wenye majina makubwa nchini.Hayo yameongelewa na Msanii dully sykes katika mahojiano.“Kanumba alikuwa ana uwezo wa hata kuchukua nauli yake ya kwenda sehemu kama Ghana kwenye tamasha la movie lakini ilimradi kujitengenezea status yake. Kwahiyo Diamond ni mtu ambaye tayari ameshajitolea kwaajili ya kuutetea muziki wetu.” Alisema Dully sykes