change the language of a blog

UNAKUMBUKA COUPLE HIZI ZILIZOBAMBA KWENYE LUNINGA



1.MZEE SMALL NA BI CHAU






















Muda mrefu sana wapo pamoja kwenye sanaa,mara nyingi ukimwona mmoja basi mwingine yupo pembeni.Hata baadhi ya matangazo ya biashara wamekuwa pamoja


2.RAY NA JOHARI

Kitambo sana tangu Kaole kwenye tamthilia hadi sasa,kwa kweli walikuwa wanabamba sana.

3.NORA NA DR.CHENI
 


Duuuh! kitambo sana enzi za kaole hizo,jamani tumetoka mbali,enzi za TV moja mtaa mzima.

3.BISHANGA NA WARIDI

















4.RICHIE NA AISHA WA MAMBO HAYO















Natamani hawa watu wafanye kazi mapema,mambo haya ni moja ya kikundi cha sanaa kilichokuwa kinabamba sana

MUAROBAINI WA BONGO MOVIES



Tansia ya filamu nchini Tanzania inakabiliwa na changamoto nyingi sana ikiwemo wizi wa kazi za wasanii unaofanywa na watu wachache waopenda kudandia treni kwa mbele.pamoja na hilo lakini suala la wasanii kuuza hati miliki za kazi zao kwa wasambazaji nalo ni tatizo kubwa sana kwani inawanyonya sana wasanii.
Baraza la sanaa Tanzania(BASATA),bodi ya filamu pamoja na mamlaka ya mapato Tanzania(TRA) kwa pamoja wakiwa wanatekeleza azma ya serikali ya kutetea na kuhakikisha haki stahiki za wasanii zinaendena sambamba na kazi nzito wanazozifanya wamesema "MUAROBAINI WA WEZI WA KAZI ZA WASANII TAYARI UMESHAIVA"
Utekelezaji rasmi utaanza januari mosi 2013.
 

KUTOKA BOLLYWOOD:KATRINA KAIF USIKU USIKU KWA RANBIR KAPOOR

RANBIR KAPOOR & KATRINA KAIF




















Hakuna ubishi kwa mastaa hawa wa filamu mpya ya Ek Tha Tiger,Salman Khan na Katrina Kaif hawana tena mahusiano ya kimapenzi,lakini swli lina kuja,Katrina na Ranbir Kapoor je?















Katriina na Ranbir walionekana saa 8 usiku wakiwa pamoja katika makazi ya Ranbir,hali inayolea minong'ono mingi sana kwa mashabiki na wapenzi wao na wengi wao wakitamani wawili hawa kuwa pamoja kwani wanapendezana
.

SAJUKI NA WASTARA "GOLDEN COUPLE" MFANO WA KUIGWA



Nadiliki kuwaiwaita wawili hawa kuwa ni "golden couple" wa miaka 10 na naamini hata wewe unakubaliana na mimi.SAJUKI(Juma kilowoko) na WASTARA ni moja kati ya wanandoa ambao ni mfano wa kuigwa duniani kote.Ndoa kama ndoa pindi wawili wnapoamua kuliendea suala hili huwekeana ahadi nzuri nzuri na naamini hakuna hata ahadi ya kukimbiana pindi mambo yatapoenda mlamba basi tukimbiane,lakini ni wangapi wanaweza kutimiza ahadi za kuishi pamoja kwenye shida na raha?
Mwanzo wa mahusiano ya Sjuki na Wastara yalitokana na mashimo ya maumivu huku kila mmoja akijitahidi kuyafukia,ila tatizo ni kwa namna gani wanaweza kufukia mashimo hayo.Wakati kila mmoja akitafuta naama sahihi ya kufukia mashimo ya maumivu ya mioyo yao yaliyosababishwa na wenzi wao wa zamani,ukaribu ukawasogeza na kijiona wana kila sababu ya kuwa pamoja na kushirikiana kufukia mashimo ya maumivu,basi na mwenyezi mungi ilisha kadilia yake mawili hawa wakawa wapenzi.
Bwana Sajuki akufanya ajizi ailpeleka posa nyumbani kwa Wastara kuhidhinisha uhalali wa kuwa wachumba.
Moja kati ya matukio ambayo kamwe hawawezi kuyasahau ni ajali ya pikipiki,siku chache kabla ya ndoa hali iliyosababisha Bi.Wastara kukatwa mguu,hofu ikiwa imemtanda,"je Sajuki atanioa na hali yangu ikwa kama hivi?"
Mwanaume kamili husisima na msimo sahihi na maamizi sahihi,bila kuyumbishwa Sajuki alisimama na kuhakikisha Wastara ndiye mwanamke wa maisha yake,ndoa ikafungwa

 


.
Maisha yao ya ndoa yalikuwa mazuri sana hali ambayo ilitafsiliwa na nyuso zao zilizo na furaha muda wote.Bibi akiwa producer wa movies.bwana director,kazi mtindo mmoja.
Mwenyezi huwapa mitihani waja wake anaowapenda,Sajuki alipata mtihani wa maradhi yaliyomsumbua sana na kubadilisha kabisa hata muonekano wake.Watanzania wake kwa waume kila mtu katika nafasi yake alimwombea Sajuki kupona na huku wengine wakitoa michango ya hali na mali.Mwanamke imara,mfano wa kuigwa,Bi.Wastara alisimama imara bega kwa bega kuhakikisha kwa hali yeyote na gharama yeyote ile mume wake anapona.Kusema ukweli alionyesha juhudi ya hali ya juu kusimamia afya ya mumewe kipenzi tena huku akiwa ni mjamzito.






















Mwenyezi mungu yu pamoja na wenye kusubiri,Sajuki afya yake ikarejea na sasa yuko fiti kalikiti na sasa wana mtoto.

















Ndugu wasomaji hebu niambieni wawili hawa hawastahiki kuitwa "GOLDEN COUPLE" WA MIAKA 10?
UPENDO na UVUMILIVU ni silaha ya ndoa.
Ndoa nyingi zinavunjika kwa sababu wanandoa wengi wana nunua ndoa,huingia wakiamini magari,nyumba na pesa huweza nunua furaha ya ndoa,kumbe wamesahau mapenzi ya kweli ndiyo msingi wa kila kitu.
Kama mnahitaji ushauri mnaweza waona hawa golden couple.