change the language of a blog

SAJUKI NA WASTARA "GOLDEN COUPLE" MFANO WA KUIGWA



Nadiliki kuwaiwaita wawili hawa kuwa ni "golden couple" wa miaka 10 na naamini hata wewe unakubaliana na mimi.SAJUKI(Juma kilowoko) na WASTARA ni moja kati ya wanandoa ambao ni mfano wa kuigwa duniani kote.Ndoa kama ndoa pindi wawili wnapoamua kuliendea suala hili huwekeana ahadi nzuri nzuri na naamini hakuna hata ahadi ya kukimbiana pindi mambo yatapoenda mlamba basi tukimbiane,lakini ni wangapi wanaweza kutimiza ahadi za kuishi pamoja kwenye shida na raha?
Mwanzo wa mahusiano ya Sjuki na Wastara yalitokana na mashimo ya maumivu huku kila mmoja akijitahidi kuyafukia,ila tatizo ni kwa namna gani wanaweza kufukia mashimo hayo.Wakati kila mmoja akitafuta naama sahihi ya kufukia mashimo ya maumivu ya mioyo yao yaliyosababishwa na wenzi wao wa zamani,ukaribu ukawasogeza na kijiona wana kila sababu ya kuwa pamoja na kushirikiana kufukia mashimo ya maumivu,basi na mwenyezi mungi ilisha kadilia yake mawili hawa wakawa wapenzi.
Bwana Sajuki akufanya ajizi ailpeleka posa nyumbani kwa Wastara kuhidhinisha uhalali wa kuwa wachumba.
Moja kati ya matukio ambayo kamwe hawawezi kuyasahau ni ajali ya pikipiki,siku chache kabla ya ndoa hali iliyosababisha Bi.Wastara kukatwa mguu,hofu ikiwa imemtanda,"je Sajuki atanioa na hali yangu ikwa kama hivi?"
Mwanaume kamili husisima na msimo sahihi na maamizi sahihi,bila kuyumbishwa Sajuki alisimama na kuhakikisha Wastara ndiye mwanamke wa maisha yake,ndoa ikafungwa

 


.
Maisha yao ya ndoa yalikuwa mazuri sana hali ambayo ilitafsiliwa na nyuso zao zilizo na furaha muda wote.Bibi akiwa producer wa movies.bwana director,kazi mtindo mmoja.
Mwenyezi huwapa mitihani waja wake anaowapenda,Sajuki alipata mtihani wa maradhi yaliyomsumbua sana na kubadilisha kabisa hata muonekano wake.Watanzania wake kwa waume kila mtu katika nafasi yake alimwombea Sajuki kupona na huku wengine wakitoa michango ya hali na mali.Mwanamke imara,mfano wa kuigwa,Bi.Wastara alisimama imara bega kwa bega kuhakikisha kwa hali yeyote na gharama yeyote ile mume wake anapona.Kusema ukweli alionyesha juhudi ya hali ya juu kusimamia afya ya mumewe kipenzi tena huku akiwa ni mjamzito.






















Mwenyezi mungu yu pamoja na wenye kusubiri,Sajuki afya yake ikarejea na sasa yuko fiti kalikiti na sasa wana mtoto.

















Ndugu wasomaji hebu niambieni wawili hawa hawastahiki kuitwa "GOLDEN COUPLE" WA MIAKA 10?
UPENDO na UVUMILIVU ni silaha ya ndoa.
Ndoa nyingi zinavunjika kwa sababu wanandoa wengi wana nunua ndoa,huingia wakiamini magari,nyumba na pesa huweza nunua furaha ya ndoa,kumbe wamesahau mapenzi ya kweli ndiyo msingi wa kila kitu.
Kama mnahitaji ushauri mnaweza waona hawa golden couple.

No comments: