Moost jay si mwingine ila ni director wa tamthilia ya GREEN MESSAGE inayorushwa na luninga ya TBC1,Moost Jay yupo katika mipango ya kunyanyua vipaji vya waigizaji
Muheza-Tanga.Mkurugenz mmiliki wa kampuni ya Moost jay entertainment Bw. Mustapha j kiroboto (Moost jay) amejipanga kunyanyua vipaji vya wasanii wa kuigiza walioko wilayani
muheza mkoani Tanga. Akiongea na mtoa habari wake Moost jay amesema kuwa
anaamini kuwa mikoa mingi ina vijana wenye uwezo wa vipaji mbalimbali ila tu
wadau wengi wa sanaa wameisahau na kujiwekeza Dar peke yake,"awamu yangu
ya kwanza nimeanzia muheza lakini pia nitaitazama mikoa mengine kama morogoro,
kilimanjaro nk. Licha ya vipaji pia Tanga ina mandhari nzuri kwa kutengeneza
michezo yenye muonekano wa kiafrika. Mustapha ana mpango wa kutengeneza
Tamthilia kali inayohusu maisha ya watu waishio nje ya miji mikuu, mistuni na
kwenye majabari.. Tamthilia hii ina tabiliwa kuja kuchukua nafasi kubwa katika
luninga zote Afrika. Jina la Tamthilia hyo litatangazwa muda si mrefu. Big up moost jay God bls u. Nae mmoja wa viongozi wa makundi
ya sanaa yaliyopo Muheza, Bw. Wiliam Kiboloma
(B4B) amesema kuwa wao wako tayari kushirikiana na kampuni ya Moost jay
entertainment katika mpango huo ili kuonyesha wadau kuwa hata mikoani vipaji
vipo, B4B amewaomba pia wadhamini wengine kufuata mfano wa moost jay.
No comments:
Post a Comment