MWIGIZAJI wa sinema za kibongo, Aunt Ezekiel Grayson
‘Gwantwa’ amenusurika kupasuliwa paji la uso kwa chupa baada ya kupigwa
mkononi...
Usiku wa kuamkia
Jumatatu, nje ya Ukumbi wa Billicanas, mwanamke aliyejulikana kwa jina
moja la Yvonne alimpiga Aunt kwa chupa tupu ya bia na kumpasua mkono wa
kushoto.
Watu walioshuhudia tukio hilo wamedai kuwa,
wakati Yvonne anatekeleza ukatili huo, Aunt alikuwa amesimama na
marafiki zake waliotajwa kwa jina moja moja, Sajenti na Rehema.
“Ndani
ya ukumbi shoo ilikuwa ikiendelea, Aunt, Rehema na Sajenti walisimama
nje, ghafla alitokea Yvonne akiwa na chupa mkononi, akailenga kwenye
paji la uso la mwenzake, bahati nzuri Aunt aliiona na kukinga mkono,”
kilisema chanzo.
Kikaendelea: Vurugu kubwa ilizuka, ilibidi shoo
ndani isimame ili kushughulia suala hilo. Aunt alikimbizwa Aga Khan,
Yvonne akapelekwa msobemsobe Kituo cha Polisi cha Oysterbay, Dar ambapo
anashikiliwa.
Baada ya taarifa hizo, juzi mchana, mwandishi wetu alifika nyumbani kwa Aunt, Mwananyamala na kumkuta ambapo alikuwa na
haya ya kusema:
“Ishu ni kweli kama mlivyosikia, lakini kule Agha
Khan sikutibiwa, niliambiwa daktari hayupo mpaka saa mbili asubuhi na
muda huo ilikuwa saa kumi alfajiri.
“Ilibidi niende kutibiwa kwa Dokta Mvungi, Kinondoni Hospitali ambako nilishonwa nyuzi sita.”
mwandishi: Madai ya Yvonne ni nini hasa?
Aunt:
Yaani hata mimi sijui, nilishangaa sana. Kwanza lengo lake lilikuwa
kunijeruhi kwenye uso, lakini niliiona chupa nikaikinga na mkono ndiyo
maana ikaniumiza.
mwandishi: Siku za nyuma uliwahi kuingia kwenye mzozo
na Yvonne kwamba unamchukulia mpenzi wake aitwaye Joff, siyo kwamba
ndiyo kisasi?
Aunt: Yale mambo yalipita, yeye ana maisha yake na mimi nina yangu.
-Risasi